Kipindi cha pili uwanja ukiwa na maji baada ya mvua kunyesha kwa muda katika dakika ya 56 Lionel Messi akafunga bao la tatu na kufanya mabao kuwa 3-1.
Dakika za lala salama dakika ya 88 Cesc Fábregas aliyetokea benchi kwa kuchukua nafasi ya Pedro katika dakika ya 73 akawaongezea bao Barcelona na kufanya 4-1.
Lionel Messi akishangilia baada ya kuifungia Barcelona bao la pili na kufanya 2-1 dhidi ya Sevilla
Messi tena akiifanyia Barcelona 3-1 dhidi ya wenyeji Sevilla
Mapema kipa Victor Valdes alifungwa na Alberto Moreno katika dakika ya 15
Wachezaji wa Sevilla wakipongezana baada ya kupata bao wakiwa wa kwanza.
Piotr Trochowski na Sanchez kwenye patashika
Hakunaga!!! Tupo kileleni tena leo!!!
Meneja wa Barcelona 'Tata' Martino akitoa maelekezo leo
Messi leo kafikisha mabao 334, na hapa akishukuru kwa yote!!
No comments:
Post a Comment