Manchester United, licha ya kutawala Mechi yote, kukosa Nafasi nyingi mno na hata kuweza kutoka nyuma kwa Bao 1-0 na kumudu kuongoza kwa Bao 2-1 walikatwa maini katika Dakika ya 94 wakati Darren Bent aliposawazisha kwa Bao laini.
Kipindi cha Pili, Man United walifanya mabadiliko kadhaa kwa kuwaingiza kina Valencia, Januzaj na Chicharito na hii ilileta uhai na waliweza kufunga Bao 2 katika Sekunde 90.
Lakini kosa kosa zao za kufunga Bao la 3 kuliwagharimu kwani bila kutarajiwa Bent aliisawzishia Fulham kwenye Dakika za Majeruhi na kupata Sare ya Bao 2-2.
Manchester United, licha ya kutawala Mechi yote, kukosa Nafasi nyingi mno na hata kuweza kutoka nyuma kwa Bao 1-0 na kumudu kuongoza kwa Bao 2-1 walikatwa maini katika Dakika ya 94 wakati Darren Bent aliposawazisha kwa Bao laini. Mechi inayofuata kwa Man United ni hapo Jumatano huko Emirates watakapoivaa Arsenal ambayo Jana ilikung’utwa Bao 5-1 na Liverpool huko Anfield.
Kipa wa United hoi!! baada ya kusawazisha Fulham katika dakika za majeruhi..
No comments:
Post a Comment