Wachezaji wa kilabu ya Chelsea Frank Lampard,Oscar na Ramirez wanaunga mkono kampeni hiyo inayoshirikisha kitengo cha kukabiliana na uhalifu nchini Uingereza pamoja na serikali ya Brazil.
Kampeni hiyo inawaonya wafuasi wa Uingereza kwamba watakabiliwa na tisho la kushtakiwa iwapo watalipa ili kulala na wasichana walio chini ya umri 18.
Taifa la Brazil linakadiriwa kuwa na nusu ya milioni ya idadi makahaba watoto wanaosimamiwa na magenge ya uhalifu na kuna hofu kwamba idadi hiyo itaongezeka wakati wa michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment