BUKOBA SPORTS

Saturday, February 8, 2014

MASHINDANO YA NGUMI NELSON MANDELA OPEN BOXING CHAMPIONSHIP YAZIDI KUNOGA KAWE


Bondia Habasi Hamisi wa Kigoma akikwepa konde la Mustafa Murinho wakati wa mashindano ya Nelson Mandela Open Championship yaliyofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam Morinho alishinda kwa point mpambano huo na kuingia fainal

Bondia Finias Genga kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Haruna Swanga wakati wa mashindano ya Nelson Mandela Openchampion ship yaliyofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam Swanga alishinda kwa TKO ya raundi ya kwanza na kufanikiwa kuingia fainal ya mashindano hayo Picha Na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Haruna Swanga akinyooshwa mkono juu kuashilia ushindi wake
Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis akisaidia kufunga mlingoti wa taa katika mashindano hayo.

Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT Mutta Rwakatare akimwelekeza ofisa habari wake Viduka jinsi ratiba ya mahindano yanavyokwenda kushoto ni Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis
Diwani wa Kata ya Kawe Othumani Kipete Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis na
Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT Mutta Rwakatare wakifatilia kwa makini Mashindano hayo

Aisha Vonialis

Na Mwandishi Wetu Kawe
Mjumbe wa maendeleo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis amesema wanawake wanatakiwa wawe na msukumo mkubwa katika kuhakikisha wanajitokeza kwenye mchezo wa masumbwi akizungumza wakati wa mashindano ya kumuenzi Rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini Nelson Mandela Open Boxing Championship yaliyofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam

Mjumbe huyo alitoa wito kuwa wanawake wanaweza hivyo wajitokeze katika kucheza mchezo wa ngumi na kuangalia mchezo huo kama michezo mingine akitolea mfano unaona katika mashindano haya wanawake ndio walio ongoza kuja kwa wingi kwa kuwa wanapenda mchezo siku zote tulizo kuwepo hapa katika viwanja hivi wanawake wanakuja kushingilia sana tu

aliongeza kwa kusema kuwa wanaomba mashilika,makampuni tasisi mbalimbali pamoja na watu binafsi kuja kusaidia mchezo wa masumbwi upate wadhamini wa kutosha kwani mashindano hayo yamekutanisha mikoa mbalimbali nchini kwa sasa hivyo wadau wote wanaombwa kujitokeza kudhamini mchezo huo


Katika mashindano hayo ya kuingia fainali bondia Mustafa Morinho alimsambalatisha Abbasi Hamisi uku Jonson Swanga akimpiga Disson Everest na Abuu Said akimdunda Frank Msindo na Haruna Swanga akimwazibu bila huluma bondia Finias Genga kwa TKO ya raundi ya kwanza

No comments:

Post a Comment