Klabu hiyo Kigogo ya Italy imethibitisha kuwa Mchezaji huyo kutoka Serbia mwenye Miaka 32 amesaini nao Mkataba lakini hawakutoboa ni wa muda gani.
Mwezi uliopita Vidic alitangaza kuondoka Man United baada kukaa Kipindi cha Miaka 8 na Nusu huku Meneja wa Man United, David Moyes, akisema uamuzi huo ulikuwa wa pande zote mbili.
Ingawa inasadikiwa mwenyewe Vidic alipendelea kubakia Man United Mkataba wake wa sasa unapokwisha mwishoni mwa Msimu huu, lakini kwa vile hakupewa Mkataba mpya aliamua kusaka Klabu nyingine.
Licha ya Vidic kutangaza kuondoka, Mchezaji huyo amebaki kuwa Nahodha wadhifa ambao amekuwa nao tangu mwanzoni mwa Msimu wa 2010/11.
Vidic alisainiwa kwa Dau la Pauni Milioni 7 kutoka Spartak Moscow na kujenga uhusiano mzuri na Rio Ferdinand kama Masentahafu bora kwenye Ligi Kuu England na wao ndio waliokuwa nguzo imara ya Man United iliyotwaa Ubingwa wa England mara 3 mfululizo kuanzia 2007 hadi 2009, kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 2008 na kufika Fainali nyingine ya UEFA CHAMPIONS LIGI Miezi 12 baadae.
Hata hivyo, Vidic alifanikiwa tena kurudi Uwanjani akiwa na Man United na kutwaa Ubingwa wa England mara mbili zaidi na mara ya mwisho ikiwa Mei Mwaka Jana wakati Meneja wa Timu hiyo, Sir Alex Ferguson, alipostaafu baada ya Miaka 26.
Five star:The big Serbian defender lifts his fifth league trophy in 2013
No comments:
Post a Comment