Wakitangaza Adhabu hiyo, FA, Chama cha Soka England, kilitoa taarifa kwenye Tovuti yao na kuelezea kuwa Adam alikanusha Mashitaka hayo lakini Jopo Huru la Marefa Watatu wa zamani kimempata na hatia na hivyo kufungiwa Mechi 3.
Tukio hilo la Adam kumkanyaga Giroud halikuonwa na Marefa wa Mechi hiyo lakini lilinaswa kwenye Video.
Hivyo, Jopo Huru la Marefa Watatu wa zamani liliupitia Mkanda huo wa Video na kuishauri FA kuwa endapo Refa angeliliona tukio lenyewe Charlie Adam angepewa Kadi Nyekundu na ndio maana FA imeamua kumfungia.
Akizungumzia Adhabu hii, Mtendaji Mkuu wa Stoke City, Tony Scholes, amesema: “Klabu kama sisi ni mara chache tunashinda Rufaa hizi! Tulitoa utetezi mzuri kuwa Adam alikuwa akitazama Mpira wakati wote na hakuona wapi anakanyaga!”
No comments:
Post a Comment