Katika mechi ya kwanza iliyochezwa nchini Zambia Twiga Stars ilifungwa mchezo huo kwa mabao 2-1 hivyo imetolewa kwa jumla ya mabao 3-2.
Ushindi huo uliipeka Twiga Stars hadi mapumziko ya kipindi cha kwanza bila kuwapa nafasi Shepolopolo waliokuwa wakijitahidi kwa kila namna ili kusawazisha.
Baada ya mapumziko timu zote zilikuwa na ushindani mkali lakini dakika ya 65 Kocha Rogasian Kaijage alifanya mabadiliko katika kikosi chake cha Twiga Stars kwa kumtoa Shelder Boniface na kumwingiza Fatuma Mustafa lakini bado haikusaidia.
Mnamo dakika ya 80 Shepolopolo walifanikiwa kusawazisha bao la kwanza kupitia kwa Suzan Banda baada ya mchezaji wa Twiga Stars Evelyn Sekikubo kumfanyia madhambi Mzambia Hellen Mubanga katika eneo la hatari.
Bao hilo lilipigwa moja kwa moja na kuingia golini, baada ya Kipa Fatuma Omar konekana kukaa nyuma ya mabeki waliokuwa wamemziba bila kuona mpira uliokuwa ukigongwa.
Aidha, dakika ya 86 Kocha Kaijage alifanya tena mabadiliko kwa kumtoa Amina Ally na kumwingiza Zena Khamis ili kuleta matunda, lakini ushindani ulikuwa mkali kila upande.
Pamoja na hayo yote, Twiga Stars ilipoteza nafasi nyingi za kufunga ambapo dakika ya 5, 7, 13, 20 walikuwa wakipiga mipira ikipaa na kutoka nje.
Kutokana na kupoteza mchezo huo, Twiga Stars watapumzika hadi mwakani katika michuano mingine.
No comments:
Post a Comment