BUKOBA SPORTS

Friday, May 16, 2014

CLIVE ALLEN: MWENYEKITI LEVY ‘SI MTU WA SOKA!’ HUKU CLIVE IKIWA PENDEKEZO LAKE KWA SASA NI CARLO ANCELOTTI!!

Mwenyekiti wa Tottenham Hotspurs, Daniel Levy, ‘Si Mtu wa Soka’ kwa mujibu wa Mchezaji na Kocha wa zamani wa Klabu hiyo, Clive Allen.
Tangu Levy aitwae Spurs Mwaka 2001, Mameneja 9 wameshaondoka hapo na wa mwisho ni Tim Sherwood ambae alifukuzwa Juzi Jumanne baada ya kuwa kitini kwa Miezi mitano tu.
Allen, Miaka 52, amemwelezea Levy kama Mafanyabiashara mzuri lakini maamuzi yake ya Kisoka ni mabovu.
Allen amedai: "Sidhani kama yeye ni Mtu wa Soka. Haya maamuzi yatakuja kumsulubu!”
Allen, ambae alikuwa Meneja wa Suprs kwa Mechi 1 tu baada ya kutimuliwa kwa Martin Jol Mwaka 2007, pia ameponda ununuzi wa Wachezaji wa Spurs wa hivi karibuni.

Amedai Spurs ina Kikosi cha Wachezaji wenye thamani kubwa lakini hamna mafanikio.
Amesema: “Ni Kikosi chenye thamani kubwa mno na Mtu lazima awajibike. Inasikitisha sana Kikosi hiki kimemaliza Ligi Nafasi ya 6 na hakiwezi kushindana na Timu zilizo 4 Bora. Lazima ufanywe uamuzi wa dira mpya ni ipi!”

Meneja wa mwisho kutimuliwa, Tim Sherwood, alijifananisha na ‘Mwalimu wa Ugavi’ baada Wachezaji wake kuambiwa na Mawakala wao kwamba Meneja huyo hatakuwepo Klabuni hapo Msimu ujao wakati yeye mwenyewe alikuwa hajui lolote kuhusu hatima yake.
Hivi sasa kuna minong’ono kuwa Spurs inalenga kuwaajiri ama Meneja wa Southampton Mauricio Pochettino au Bosi wa Ajax Frank de Boer kuziba pengo la Sherwood. 
Pendekezo la Allen kwa sasa ni Ancelotti


MAMENEJA CHINI YA LEVY:
-George Graham
-Glenn Hoddle
-David Pleat
-Jacques Santini
-Martin Jol
-Juande Ramos
-Harry Redknapp
-Andre Villas-Boas
-Tim Sherwood

 

No comments:

Post a Comment