Usiku huu, huko Juventus Stadium, Jijini Turin, Nchini Italy, Benfica walitoka 0-0 na Sevilla katika Fainali ya EUROPA LIGI kwa Dakika 90 na Dakika 30 za Nyongeza ilibaki 0-0 na Sevilla walitwaa Ubingwa kwa Mikwaju ya Penati 4-2.
Bela Guttman, ambae ndie alimsaini Lejendari wa Ureno Eusebio, aliipa Benfica Mataji kadhaa ya Nchini Ureno na Mawili ya Ulaya, lakini aliondoka Klabu hiyo kwa ugomvi mkubwa kutokana na mvutano wa Malipo yake na kuilaani Benfica kwa kutamka haitatwaa Taji lolote Ulaya kwa Miaka 100.
Tangu wakati huo Benfica wameshashindwa Fainali 8 za Ulaya ikiwemo ile ya Kombe la Ulaya la Mwaka 1988 walipofungwa kwa Penati na PSV na Msimu uliopita kutolewa na Chelsea kwenye Fainali ya EUROPA LIGI huku Bao la ushindi la Chelsea likifungwa Dakika ya 93 na Branislav Ivanovic.
Kwenye Fainali hii, Penati za Sevilla zilifungwa na Bacca, Mbia, Coke na Gameiro na Benfica kukosa Penati mbili zilizookolewa na Kipa Beto, Mzaliwa wa Lisbon, Ureno, ambazo zilipigwa na Cardozo na Rodrigo wakati Luisao na Lima waliifungia Benfica.
No comments:
Post a Comment