Alama ya chaki ya kupulizia (spray) ni moja ya ingizo jipya kwenye michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil. Tayari refa ameshaitumia mara ya kwanza kwenye mechi ya ufunguzi kati ya Brazil na Croatia usiku wa kuamkia leo, pale refa alipochora kwa kupulizia na kuweka alama wapi wachezaji wasimame wakati wa kupigwa mpira wa adhabu (pichani chini), ili kuthibiti zogo la wachezaji, ama wapi mpira uwekwe kabla ya kupigwa. Chaki hiyo, ambayo huyeyuka baada ya dakika chache, ilianza kutumika mwaka jana kwenye kombe la Klabu Bingwa ya Dunia ambapo huko Argentina na Brazil ilitumika kwa Misimu kadhaa iliyopita.
Usiku Alama hii ilitumika
Usiku Alama hii ilitumika
No comments:
Post a Comment