BUKOBA SPORTS

Friday, June 13, 2014

CAMEROON: TIMU YA KWANZA AFRIKA KUCHEZA ROBO FAINALI YA KOMBE LA DUNIA


Na Baraka Mbolembole
Senegali ifikia hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia mwaka 2002 katika nchi za Korea Kusini na Japan na kuwa timu ya pili ya Afrika kufika hatua hiyo baada ya Cameroon kufanya hivyo mwaka 1990 nchini Italia.
Senegal kama ilivyo kwa Cameroon ilifanya vizuri katika michuano yake ya kwanza ya fainali hizo kubwa zaidi za soka duniani. Wakati Ghana ilikuwa timu ya tatu ya Afrika kufika hatua hiyo . Wakicheza fainali za pili mwaka 2010, Black Stars ilifika hatua ya robo fainali na kuondolewa kwa changamoto ya mikwaju ya penalty na Uruguay. Saa moja usiku wa leo, miamba wa soka Afrika wataanza kutupa karata yao ya kwanza kwa kushuhudia Cameroon wakipambana na timu ya Mexico kutoka Marekani Ya Kati.
Cameroon ilifuzu kwa fainali za kombe la dunia kwa mara ya kwanza mwaka 1990 katika fainali ambazo zilifanyika nchini Italia. Cameroon walipangwa katika kundi moja na waliokuwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Argentina na Romania na Urusi na walimaliza kama vinara wa kundi baada ya kuifunga Argentina katika mchezo wa ufunguzi kwa goli la mshambuliaji, Francois Omani Bjyik, wakaicha Romania katika mchezo wa pili kwa magoli 2-1 ingawa walipoteza dhidi ya Urusi kwa magoli 4-0 katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi.

Senegal maarufu kwa jina la `Simba wateranga` walifika robo fainali mwaka 2002.
Wakaichapa Colombia kwa magoli 2-1 katika mchezo wa hatua ya 16 na kuwa timu ya kwanza kutoka barani Afrika kufika hatua ya juu zaidi katika michuano hiyo. Walitinga robo fainali kwa msaada wa mshambiliaji Roger Millar ambaye alifunga magoli yote mawili akiwa na umri wa miaka 38.
Goli la David Platt katika dakika ya 25 lilifutwa na Emmanuel Kunde kabla ya Eugene Ekeke kuongeza goli lingine wakati Cameroon ilipotoka nyuma na kuongoza dhidi ya England katika mchezo war obo fainali. Magoli hayo yalifungwa katika dakika za 61 na 66 kabla ya Gery Lineker kusawazisha katika dakika ya 83 na kufanya mchezo huo kwenda katika hatua ya dakika 30 za nyongeza. Na katika dakika ya 105, England wakapata mkwaju wa penalty na Lineker akafunga goli la ushindi ambalo lilihitisha mafanikio ya ‘ Simba Wasioshindika’ katika fainali zao za kwanza.
Miaka minne iliyofuata nchini Marekani, Cameroon walipangwa katika kundi la pili sambamba na Brazil, Sweden na Urusi. Walianza na sare ya kufungana magoli 2-2 na Sweden, wakachapwa magoli 3-0 na Brazil na wakakutana na kipigo kikubwa zaidi mbele ya Urusi baada ya kutandikwa magoli 6-1. Walichoambulia katika fainali za mwaka 1994 ni rekodi iliyowekwa na mshambuliaji, Rogar Millar ambaye alifunga goli la kufutia machozi la Cameroon akiwa na umri wa miaka 42 na kuweka rekodi ya mfungaji mwenye umri mkubwa zaidi iliyodumu hadi sasa.

Kikosi cha Cameroon kilichofika robo fainali mwaka 1990
Cameroon waliondolewa katika hatua ya makundi wakiwa na pointi moja tu. Walifuzu kwa mara ya tatu katika fainali za Ufaransa, mwaka 1998 na wakaangukia katika kundi la pili sambamba na Italia, Chile na Austria. Walitoa sare dhidi ya Chile na Austria na kuifunga Italia kwa magoli 3-0. Katika fainali zao za nne katika nchi za Korea Kusini na Japan, 2002 walipangwa na Ujerumani, Ireland na Saudi Arabia. Walianza michuano kwa sare ya kufungana goli 1-1 na Ireland wakaishinda Saudi Arabia kwa goli 1-0 lakini wakajikuta wakipoteza mchezo wa mwisho dhidi Ujerumani baada ya kulazwa magoli 2-0.
Waliishia katika hatua ya makundi kwa mara nyingine. Mabingwa hao wa zamani wa Afrika walifuzu kwa fainali za Afrika ya Kusini, miaka minne iliyopita baada ya kushindwa kufuzu kwa michuano ya mwaka 2006, nchini, Ujerumani. Walipangwa na Denmark, Japan na Uholanzi. Walifungwa na Denmark kwa magoli 2-1 wakaishinda Japan kwa goli 1-0 katika mchezo wa pili kabla ya kupoteza mchezo wa mwisho dhidi ya Uholanzi baada ya kulala kwa magoli 2-1 na wakaishia hatua ya makundi.

Samuel Eto`o alishangilia kwa staili ya kibabu kinachotembelea mkongojo baada ya kufunga bao katika mechi ya kirafiki dhidi ya Ujerumani, hii ni kejeli kwa Jose Mourinho aliyemuita mzee. Leo nyota huyo anaiongoza Cameroon kombe la dunia.
Kuelekea mchezo wa jioni ya leo dhidi ya Mexico, kikosi cha Cameroon chini ya kocha, Voljer Finke kinakabiliwa na changamoto kubwa kuhakikisha wanapata ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu kwa hatua ya mtoano. Baada ya ushindi wa Brazil dhidi ya Croatia, Cameroon itakuwa na nafasi nzuri ya kufuzu kwa hatua ya 16 kama watapata ushindi jioni ya leo. Ratiba inaonesha watakutana na Croatia katika mchezo wa pili kabla ya kumaliza na Brazil hivyo ushindi katika mchezo wa leo ni muhimu sana kama wanataka kufuzu kwa hatua inayofuata. Mshambuliaji, Samuel Eto’o atakuwa akicheza fainali zake za tatu za kombe la dunia na nchi yake itakuwa ikicheza fainali za sita. Cameroon wanauzoefu wa kutosha wanaweza kutinga hatua ya 16 bora wakishinda mchezo wa leo dhidi ya Mexico.

No comments:

Post a Comment