BUKOBA SPORTS

Monday, June 9, 2014

SONY: UCHUNGUZI UFANYWE KUHUSU QATAR 2022

Rais wa shirikisho la Soka duniani Sepp Blatter
Kampuni kubwa ya kielektroniki inayofadhili michuano ya kombe la dunia Sony imetaka uchunguzi kufanywa kuhusiana na madai ya ufisadi wakati wa kutolewa kwa kandarasi ya kuandaliwa kwa michuano ya kombe la dunia nchini Qatar mnamo mwaka 2022.
Gazeti moja la Uingereza Sunday Times lilinukuliwa likisema kuwa afisa mkuu wa shirikisho la FIFA kutoka Qatar Mohammed Bin Hammam alilipa mamilioni ya madola kama hongo ili nchi yake iungwe mkono katika maandalizi ya mechi hizo.
Kamati ya maandalizi ya Qatar hatahivyo imepinga kufanyika kwa makosa yoyote.
Gazeti hilo hii leo linadai kwamba bwana Bin Hammam alitumia ushawishi wake kuhakikisha kuwa taifa lake linaanda michuano hiyo kupitia mkutano aliopanga kati ya maafisa wakuu wa FIFA na familia ya kifalme ya Qatar.

No comments:

Post a Comment