KAMISHENI ya ngumi za kulipwa Tanzania TPBC, inataraji kufanya mkutano wa kujadili na kupitisha rasimu ya chama hicho, ili kuhakikisha sheria na kanuni zinazopitishwa zinaeleweka kwa mabondia ambao ndio wadau wakuu wa mchezo huo.
Mkutano huo unatarajia kufanyika Juni 22 mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo sanjari na mambo mengine utatoa mafunzo kwa mabondia juu ya masuala mbalimbali yakiwemo sheria na kanuni za mchezo wa ngumi.
Rais wa TPBC, Chaurembo Palasa amedai kuwa baadhi ya mabondia wamekuwa wakipigana masumbwi pasipokuwa na ufahamu wa kutosha wa sheria za masumbwi hivyo kusababisha fujo au kupoteza haki yao wawapo ulingoni.
Chaurembo Palasa ambaye pia ni bondia wa zamani wa ngumi za kulipwa alisema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo mabondia katika nyanja mbalimbali za kisheria.
No comments:
Post a Comment