BAO za Dakika ya 38 na 90 zimewapa ushindi Mabingwa Manchester City walipocheza Ugenini na Newcastle huko Saint James Park katika Mechi yao ya kwanza kabisa ya Ligi Kuu England Msimu mpya wa 2014/15.
David Silva ndie aliefunga Bao la Kwanza baada ya kutengenezewa vizuri na Edin Dzeko na la Pili kupachikwa katika Dakika za Majeruhi na Sergio Aguero alieingizwa Dakika ya 83 kumbadili Edin Dzeko.
Mechi inayofuata kwa Man City kwenye Ligi ni ya Nyumbani Uwanjani Etihad hapo Jumatatu Agosti 25 watakapowavaa Liverpool.
VIKOSI:
Newcastle: Krul, Janmaat, Williamson, Coloccini, Dummett, Colback, Anita, Sissoko, Cabella, Gouffran, Riviere.
Subs: Aarons, Perez, Haidara, Elliot, Obertan, Steven Taylor, Abeid.
Manchester City: Hart, Clichy, Demichelis, Kompany, Kolarov, Fernando, Toure, Nasri, Jovetic, Silva, Dzeko.
Subs: Zabaleta, Milner, Caballero, Jesus Navas, Aguero, Fernandinho, Boyata.
Referee: Martin Atkinson
No comments:
Post a Comment