December mwaka jana Andrea Sambu naMusanduki Mohamed walifikia viwango ‘TAKATIFU’ vya ushiriki wa Commonwealth Games ila kwa sababu ya “Agenda yao ya Siri” hawakujumuishwa timu ya Glasgow.
Hivyo kwa ubabe kabisa RT walikataa bila maelezo ni kwa nini waliwaacha wanariadha hao.
Hivyo Tanzania tumekosa medali kwa sababu zifuatazo;
- Waliamua kumwacha Andrea Sambu kwa sababu aliyemuandalia mbio za China ni Wilhelm Gidabuday ambaye RT wanaona ni adui wao mkubwa sababu ya kuwa mkweli
- Je watanzania wakose MEDALI kwa sababu ya ubabe wa viongozi wa RT na hatimaye Tanzania kukosa sifa wakati FEDHA ZA WALIPA KODI zimetumika ili taifa liondokane na aibu.
- Ifahamike wazi bila kupepesa kwamba RT inaongozwa na viongozi FEKI sababu hawakuchaguliwa kwa katiba ya RT wala kwa SHERIA # 12 ya BMT iliyotungwa na BUNGE 1967.
- ANDREA SAMBU SIPE
Fedha alizotoa Waziri Membe hazikuingizwa account ya RT; Je Mheshimiwa Membe aliweka fedha hizo kwenye box akawakabidhi rundo la minoti? TUNGEPENDA MEMBE AFAFANUE!
- Vinginevyo nia yake njema inaweza kutafsiriwa vinginevyo maana hivi sasa siasa imeshaingilia viwanja vya michezo ndiyo maana DC Mtaka anatafuta CV kupitia Chama Cha Riadha (RT).
- Je timu ya riadha ya kwenda kambi za nje ilichaguliwa kwa VIGEZO GANI? Bilashaka Waziri Membe angelihakikisha kwamba fedha anazozitoa zinakwenda kufanya ‘Intended Mission’.
- Pia Waziri Membe afahamu kwamba kuna watu watatu ambao walifanikisha‘Proposal’ aliyoletewa ambayo ilikuwa na neno “SPORTS DIPLOMACY” watu hao ni Mwalimu Samwel Tupa, Wilhelm Gidabuday na Thabit Bashir.
- Inashangaza sana kwamba William Kallaghe anaficha ukweli wa ushiriki wa wadau wa riadha waliotumia muda wao mkubwa kuandaa mchanganuo ambao ndiyo sasa unajulikana kwa jina zuri sana la “SPORTS DIPLOMACY”
“WANARIADHA WOTE KWA SAUTI MOJA TUNAMTAKA WAZIRI MEMBE AWASHIRIKISHE WADAU MUHIMU SIKU RIPOTI YA GLASGOW INAPOWASILISHWA ILI KILA ALIYE MTAALAM WA MICHEZO APATE KUTOA WAZO LAKE KWA NIA NJEMA YA KUBORESHA TIMU YETU SIKU ZA USONI.
No comments:
Post a Comment