BUKOBA SPORTS

Friday, August 8, 2014

KINDA' JAMES WILSON WA MANCHESTER UNITED AITANDIKA PEKE YAKE MANCHESTER CITY 4-1 NA KUBEBA KOMBE!


KINDA wa Manchester United,James Wilson amemkumbusha Louis van Gaal umuhimu wake kwa kufunga mabao yote manne katika ushindi wa 4-1 dhidi ya mahasimu wao wakubwa Manchester City.
Timu hizo mbili hasimu zilikutana jana usiku katika mchezo wa fainali wa kombe la 'Manchester Senior Cup'.
Wilson alifunga mabao mawili katika mechi yake ya kwanza ya ligi kuu dhidi ya Hull City msimu uliopita chini ya kocha wa muda Ryan Giggs, lakini hakuchukuliwa na Van Gaal katika ziara ya hivi karibuni ya maandalizi ya msimu nchini Marekani. Lakini katika mechi ya jana iliyotazamwa na Manuel Pellegrini, Wilson alionesha kiwango kikubwa na kubeba kombe hilo la 'Senior Cup' baada ya kufunga mabao mawili katika kila kipinidi na kuifanya United ishinde ikitokea nyuma.


James Wilson alikuwa shujaa wa United, akifunga mara nne baada ya Man City kutangulia kupata bao la kuongoza.

Katika mechi hiyo vijana walipeana changamoto kubwa na kuonesha jinsi gani wamebarikiwa kucheza soka.

Jordi Hiwula, katikati kulia, akimpanda Devante Cole, kulia, baada ya kuifungia Man City bao la kuongoza
VIKOSI:
Kikosi cha Manchester City:
Gunn, Bossaerts, Maffeo, Bryan (Smith-Brown 46), Angelino, Glendon, Ntcham (Horsfield 53), Fofana, Cole, Pozo (Ambrose 68), Hiwula
Wachezaji: O'Brien, Bytyqi.
Mfungaji wa goli: Hiwula.
Kikosi cha Manchester United: J Pereira; Vermijl, McNair, Thorpe, Varela; Janko, Pearson, Rothwell, Lawrence; A Pereira; Wilson
Wachezaji wa akiba: O'Hara, Harrop, Goss, Willock, Evans
Mfunagi wa magoli: Wilson (4).
Watazamaji: 3,261.

No comments:

Post a Comment