BUKOBA SPORTS

Monday, August 18, 2014

USAJILI: WAMILIKI WA MARCOS ROJO WAKWAMISHA USAJILI WAKE KUELEKEA MANCHESTER UNITED.

UGOMVI kati ya Wamiliki wa Mchezaji wa Kimataifa wa Argentina unawavuruga Manchester United katika azma yao ya kumsajili Beki wa Sporting Lisbon Marcos Rojo.
Manchester United imeshatoa Ofa ya Pauni Milioni 16 kumnunua Mchezaji huyo mwenye uwezo mkubwa kucheza kama Sentahafu au Fulbeki wa kushoto na ambae Meneja Louis van Gaal anamwona anafaa sana kwa Mfumo wake mpya wa 3-4-1-2.

Lakini Dili hii imekumbwa mizengwe na vikwazo vikubwa kuhusu mgao wa Fedha kwa Wamiliki wa Mchezaji huyo.
Rojo alihamia Sportung Lisbon Mwaka 2012 akitokea Spartak Moscow na Kampuni ya Doyen Sport ililipa Asilimia 75 na Sporting Lisbon kulipa Asilimia 25 ya Ada ya Uhamisho wake.

Hivi sasa inadaiwa Sporting Lisbon wanataka kumuuza Mchezaji huyo kwa Pauni Milioni 24 ili wao wapate mgao mkubwa zaidi na inasemekana wamewaambia Man United hawana haja ya kuzungumza na Doyen Sport kwa vile Dili ya Rojo ilifanywa na Utawala uliopita wa Klabu hiyo na wao hawautambui.
Doyen Sports imeijia juu Sporting Lisbon na kutaka Mchezaji huyo auzwe kwa Man United na kutishia kuchukua hatua za Kisheria ikiwa Klabu hiyo ya Ureno haitawalipa Asilimia 75 ya Ofa yeyote inayokataliwa.
Mkataba kati ya Doyen Sports na Sporting Lisbon unasema ikiwa mmoja kati yao atagomea kuuzwa Mchezaji huyo basi yule aliegoma anapaswa kumlipa mwingine Asilimia zilezile za umiliki wa Mchezaji huyo kulingana na Ofa iliyotolewa na kukataliwa.
Kwa sababu Sporting Lisbon ndio wanagoma kumuuza Rojo basi wao wanapaswa kuilipa Doyen Sports Pauni Milioni 12.

Hali hii imeifanya Man United kusita kujitumbukiza kwenye mgogoro huo lakini inatarajiwa mazungumzo yataendelea Jumatatu huku kukiwa na ripoti kuwa Sporting Lisbon watakubali kumaliza Dili hii ikiwa watapewa Mchezaji mmoja kwa Mkopo na wao wamewataja Anderson au Nani.

Tangu Wiki iliyopita Rojo amegoma kufanya Mazoezi na Sporting Lisbon akishinikiza Klabu hiyo imruhusu ahamie Man United na inasemekana ameadhibiwa kwa mgomo huo.
Hata hivyo, ikiwa Dili hii itakamilika Man United wanapaswa kuzingatia Sheria za Usajli Wachezaji England ambazo zinataka Mchezaji amilikiwe moja kwa moja na Klabu husika na hii itawafanya Man United kupaswa kununua haki zake zote za umiliki wa Rojo.

No comments:

Post a Comment