BUKOBA SPORTS

Saturday, October 18, 2014

ARSENAL 2 vs 2 HULL CITY, DANNY WELBECK AIOKOA GUNNERS EMIRATES LEO! ASAWAZISHA BAO KATIKA DAKIKA ZA LALA SALAMA.


Alexis Sánchez ndie aliyeanza kuliona lango la Hull katika dakika ya 13, Dakika nne baadae katika dakika ya 17 Mohamed Diame aliisawazishia bao na kufanya 1-1. Kipindi cha pili mwanzoni dakika ya 46 Abel Hernández aliwachoma Gunners bao la pili na kufanya kibarua kuwa kugumu kwa Arsenal wakitafuta bao la kusawazisha kwa bidii zote.
Katika dakika za lala salama za kipindi cha pili Danny Welbeck aliwasawazishia bao Arsenal kwenye dakika ya 90' +1 na mtanange kumalizika kwa sare ya 2-2.

No comments:

Post a Comment