BUKOBA SPORTS

Tuesday, October 14, 2014

BRAZIL 4 vs 0 JAPAN, NEYMAR ANATISHA! AFUNGA HAT-TRICK AKIFUNGA BAO ZOTE NNE!

Leo kwenye Mechi ya Kimataifa ya Kirafiki iliyochezwa huko Stadium of Singapore Nchini Singapore, Neymar ameifungia Nchi yake Brazil Bao zote walipoitwanga Japan 4-0.
Bao hizo zimemfanya Neymar afikishe Bao 40 katika Mechi 58 alizochezea Brazil.
Hadi Mapumziko Brazil walikuwa mbele kwa Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 18 la Neymar Da Silva anaechezea Klabu ya Barcelona huko Spain. 
Neymar akifanya mambo yake..The Barcelona forward almost got on the scoresheet early on, bending a beautiful free kick over the wall only to see it hit the crossbarKipindi cha Pili Neymar aliongeza Bao 3 nyingine katika Dakika za 48, 77 na 81. 
Hii ni Mechi ya Pili ya Kirafiki kwa Brazil huko Bara la Asia baada ya Jumamosi kuichapa Argentina Bao 2-0 huko Beijing, China.
Kocha mpya wa Brazil, Dunga, sasa amepata ushindi wake wa 4 mfululizo katika Mechi zake 4 za kwana.

VIKOSI:
BRAZIL (4-2-3-1):
Jefferson; Danilo, Miranda, Gil, Filipe; Luiz Gustavo, Elias; Willian, Oscar, Neymar; Diego Tardelli.
Akiba: Rafael, Marcelo Grohe, Mario Fernandes, Juan, Dodo, Romulo, Souza, Everton Ribeiro, Kaka, Coutinho, Robinho.
JAPAN (4–3-3): Kawashima; Ota, Shiotani, Morishige, Sakai; Morioka, Taguchi, Shibasaki; Okazaki, Kobayashi, Tanaka.
Akiba: Nishikawa, Gonda, Mizumoto, Nagatomo, Nishi, Suzuki, Hosogai, Honda, Havenaar, Kakitani, Muto. 

REFA: A. A'Qashah‎ [Singapore]

No comments:

Post a Comment