BAADA ya TFF kumfungia Dokta Damas Ndumbaro Miaka 7 kutojihusisha na Soka na kumpiga Faini juu, Mwanasheria huyo ameibuka na kudai ‘TFF haina mamlaka dhidi yake.’
Adhabu ya Dokta Ndumbaro ilitolewa naKamati ya Nidhamu ya TFF lakini yeye amepinga na kudai TFF ilipaswa kuainisha hayo makosa anayotuhumiwa kuwa nayo kwa kuvitetea Vilabu vya Ligi Kuu Vodacom, na kisha kuwasilisha malalamiko yao kwenye Kamati ya Maadili ya Mawakili au kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kiini cha mzozo huu ni baada ya Rais wa TFF, Jamal Malinzi, kuagiza kila Klabu kukatwa Asilimia 5 ya Mapato yao kutoka kwa Wadhamini wa Ligi Kuu Vodacom na Ndumbaro kukaririwa kuwa Klabu za Ligi hiyo zimemuagiza kupinga jambo hilo huku akidai wanatafuta Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kuunga mkono Kura ya kutokuwa na imani na Malinzi.
TFF ikaamua kufungua mashtaka kwenye Kamati ya Nidhamu dhidi ya Dokta Damas Ndumbaro kwa vile ni Mjumbe wa Bodi ya Ligi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba.
Hatua ya Dokta Ndumbaro kudai TFF haina mamlaka kumhukumu imewashangaza Wachambuzi wa Soka waliodai hakusulubiwa yeye kama Mwanasheria anaetetea Mtu, Klabu au Mamlaka nyingine bali ni Wadhifa wake ndani ya Soka ndio umemhukumu na hatimae kumpa Adhabu hiyo.

No comments:
Post a Comment