Man United, chini ya Meneja Louis van Gaal, Jumatatu Usiku watakuwa Ugenini kucheza na West Bromwich Albion na kufuata Mechi mbili mfululizo dhidi ya Vinara wa Ligi Chelsea na kisha Mabingwa na Mahasimu wao wakubwa Manchester City.
Akiongea na Tovuti ya Man United, ManUtd.com, Neville, ambae sasa ni Kocha Msaidizi wa England na pia Mchambuzi kwenye TV ya Sky Sports, amesema Mechi hizi ndio kipimo halisi kwa Man United ilikofikia.
Amesema: “Huu ni wakati wa kusisimua. Ni Wiki muhimu zinakuja na Gemu dhidi ya West Brom, Chelsea na City ni kubwa. Na hizi zitatujulisha Timu hii iko wapi.”
Aliongeza: “Itakuwa ngumu kwa United kuingia UEFA CHAMPIONS LIGI na wakiweza ni mafanikio makubwa. Kwa sasa tuko Nafasi ya 4 lakini tutajijua Wiki chache zijazo. Hatujacheza na Timu ngumu. Najua Everton unaweza kusema ni Timu ngumu lakini Mechi na Chelsea na City ndio kipimo sahihi kujua Timu iko wapi.”
Neville amesema: “Nimetazama Mechi nyingi za City na Chelsea na Chelsea ndio bora kwa mbali. Lakini napenda kufikiria United ndio Klabu pekee inayoweza kubwaga Timu ngumu. Hata wakati wetu ambao tulikuwa si wazuri tuliweza kuwabwaga wazuri kama ile Arsenal ‘Isiyofungika’ na Chelsea na nakumbuka Darren Fletcher ndie alifunga Bao katika Mwaka wa kwanza wa Jose Mourinho pale Chelsea!”
Neville aliendelea: “Kuelekea Oktoba 26, Chelsea watatoka kucheza Ulaya na najua Man United wataisumbua Chelsea. Itakuwa Gemu ngumu kwao na Jose Mourinho anajua hilo!”
Mechi 3 zijazo:MAN UNITED
Jumatatu Oktoba 20
22:00 West Brom v Man United
Jumapili Oktoba 26
19:00 Man United v Chelsea
Jumapili Novemba 2
16:30 Man City v Man United
No comments:
Post a Comment