RAY PARLOUR: ARSENAL ITEGEMEE KUMALIZA NAFASI YA 3 AU 4 TU!
KIUNGO wa zamani wa Arsenal Ray Parlour amesema Msimu huu Klabu yake hiyo ya zamani isiwe na matumaini yeyote zaidi ya kumaliza Nafasi ya 3 au ya 4 kwenye Ligi Kuu England. Matokeo hayo yamewaacha Arsenal wakiwa Nafasi ya 6 wakiwa Pointi 11 nyuma ya Vinara Chelsea na Pointi 6 nyuma ya Timu ya Pili, Manchester City, ambao ni Mabingwa Watetezi.
Hivi sasa huko England ipo dhana kubwa kuwa mbio za Ubingwa kwa Msimu huu ni kati ya Timu mbili tu, Chelsea na Man City, huku Arsenal, Man United, Liverpool na Tottenham zikitajwa kuwa ndizo zitakazogombea Nafasi za 3 na 4.
Ray Parlour, akiongea kwenye Kipindi cha Weekend Sports Breakfast cha talkSPORT, amesema: “Nadhani Arsenal wanapigania Nafasi ya 3 au ya 4. Ukiwatazama Chelsea na City wapo Ligi tofauti na Arsenal. Wako juu ya Timu zote Arsenal, Man United, Liverpool na Tottenham. Hizi ndio zinapigania Nafasi mbili, wanapigania Nafasi za 3 na 4!”
Aliongeza: “Chelsea wanalazimisha matokeo. Wanacheza kwa nguvu kupata matokeo na City ni wazuri kama Aguero atacheza kama walipoifunga Spurs 4-1!”
Jana City waliichapa Tottenham Bao 4-1 na Bao zote kufungwa na Sergio Aguero.
No comments:
Post a Comment