Mark Clattenburg hatachezesha Mechi yeyote ya Ligi Kuu England Wikiendi hii inayokuja kwa kuvunja miiko ya Marefa huko England.
Refa Clattenburg Jumamosi iliyopita alichezesha Mechi ya Ligi Kuu England huko The Hawthorns ambapo Wenyeji West Bromwich Albion walitoka Sare 2-2 na Crystal Palace.
Kufuatia Mechi hiyo ikaibuka Stori kuwa Refa huyo alikiuka maadili ya Marefa huko England na hivyo kutemwa kuchezesha Mechi.
Kwa mujibu wa Kanuni za Marefa huko England, Refa wa Mechi pamoja na Wasaidizi wake wanatakiwa wasafiri pamoja wakienda kwenye Mechi waliyopangiwa na hii ni kwa sababu ya kiusalama na kulinda maadili.
Lakini kwenye Mechi hiyo Refa Clattenburg, kwa mujibu wa Magazeti ya England Daily Mail na the Sun, alisafiri kwenda huko The Hawthorns peke yake na kuondoka baada ya Mechi hiyo akiwa peke yake kwa sababu alitaka awahi kwenda kwenye Shoo ya Muziki.
Vile vile vyanzo vya habari hizi vimedai pia kuwa Refa Clattenburg aliongea na Meneja wa Crystal Palace Neil Warnock baada ya Mechi hiyo wakiwa peke yao nje ya Uwanja yeye akiwa ndani ya Gari lake kitu ambacho ni kinyume na Kanuni za Ligi Kuu ambazo zinaruhusu Refa kuongea na Meneja wa Timu wakati yuko pamoja na Wasaidizi wake wote ama akiwa amepata ruhusa maalum na Chombo cha Marefa PGMO, Professional Game Match Officials.

No comments:
Post a Comment