BUKOBA SPORTS

Monday, October 13, 2014

WAKALA ATEMA CHECHE!! UKIMTAKA RONALDO TOA EURO BILIONI 1!

WAKALA wa Cristiano Ronaldo ambae ndie Mchezaji Bora Duniani amesema yeyote anaetaka kumnunua basi awe tayari kulipa kitita cha Euro Bilioni 1.
Jorge Mendes, ambae ndie Wakala wa Ronaldo, amesema Mkataba wa Staa huyo na Real Madrid una kipengele kinachomruhusu kuhama wakati wowote ikiwa tu Euro Bilioni 1 italipwa.
Hivi karibuni Ronaldo amevumishwa sana kuihama Real na kurudi Klabu yake ya zamani Manchester United.

Lakini Mendes amesema: “Man United ipo moyoni mwa Ronaldo na yeye anaheshimu sana Watu wanaoonyesha mapenzi kwake lakini atabaki Real.”
Mapema Mendes alikiri kuwa Siku hizi hapati tena Simu za kumuulizia Ronaldo kwani wote sasa wanajua haiwezekani kumng’oa Real.
Cristiano Ronaldo

No comments:

Post a Comment