Nyuma ya Southampton wapo Mabingwa Watetezi Manchester City ambao wako Pointi 8 nyuma ya Chelsea.
Jumapili, Arsenal walitwangwa 2-1 na Swansea na sasa wapo Nafasi ya 6 wakiwa Pointi 12 nyuma ya Chelsea.
Wenger ameeleza: “Wakiendelea hivi, inaonyesha hakuna atakaeikamata Chelsea! Kwa sasa hakuna anaeonyesha hivyo!”
Jumamosi, wakiwa huko Anfield, Chelsea walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuichapa Liverpool Bao 2-1.


Ligi Kuu England sasa imesimama kupisha Mechi za Kimataifa na itarejea tena kilingeni Jumamosi Novemba 22 na Siku hiyo Arsenal wako kwao Emirates kucheza na Manchester United.
No comments:
Post a Comment