BUKOBA SPORTS

Tuesday, November 11, 2014

OSCAR AJIFUNGA, ASAINI MKATABA WA KUMKALISHA CHELSEA HADI 2019

Kiungo wa Brazil Oscar amesaini Mkataba mpya Chelsea utakaomweka hadi Mwaka 2019.
Oscar, mwenye Miaka 23, alijiunga Chelsea Mwaka 2012 akitokea Klabu ya Brazil Internacional na kusaini Mkataba wa Miaka Mitano na kuiwezesha Chelsea kutwaa Kombe la EUROPA LIGI katika Msimu wake wa kwanza tu.

Oscar, ambae aliichezea Nchi yake Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwezi Juni na Julai, ameshaichezea Chelsea mara 92 na kufunga Bao 27.
Msimu huu amecheza Mechi 15 na kufunga Bao 4.

No comments:

Post a Comment