BUKOBA SPORTS

Saturday, November 22, 2014

BAYERN MUNICH 4 vs 0 TSG HOFFENHEIM

Bayern Munich, wameendeleza kutoa dozi kwa kuichapa Hoffenheim 4-0 kwenye Mechi ya Ligi hiyo huku Borussia Dortmund wakiutupa uongozi wa Bao 2-0 na kutoka Sare 2-2.Kwenye Mechi waliyocheza kwao Allianz Arena Jijini Munich, Bayern waliipiga Bao 4-0 Hoffenheim kwa Bao za Mario Gotze, Robert Lewandowski, Arjen Robben na Sebastian Rode. Bao la kwanza lilifungwa na Mario Götze dakika ya 23 Robert Lewandowski alipachika bao la pili dakika ya 40 na kupindi cha pili kumalizika kwa 2-0. 
Kipindi cha pili Arjen Robben aliwachapa bao la tatu dakika ya 82 na Sebastian Rode kumaliza mchezo kwa kuwachapa bao la nne na kufanya 4-0 dakika dakika za lala salama dakika ya 86 na mchezo huo kumalizka kwa bao 4-0. Hoffenheim walimaliza wakiwa Mtu 10 kufuatia Kadi Nyekundu kwa Adam Szalai katika Dakika ya 90.
Mchezo huo uliangaliwa na mashabiki 71,000 katika Uwanja huo leo jumamosi.

No comments:

Post a Comment