Baada ya kutumia zaidi ya Pauni Milioni 150 na pia kuvunja Rekodi ya Klabu kwa kumsaini Angel Di Maria kwa Pauni Milioni 59.7 kutoka Real Madrid mwanzoni mwa Msimu, Ed Woodward amesema hawana papara kusajili Wachezaji wapya.
Amesema: “Hatupo Sokoni kutafuta Kiraka wa muda mfupi. Lakini tunao walengwa wetu tunawaowataka mwishoni mwa Msimu. Ikitokea yeyote kati ya hao anaweza kupatikana Januari, kitu ambacho adimu, tutachukua hatua. Lakini uwezekano ni finyu.”
Mwanzoni mwa Msimu, Man United iliwanunua Ander Herrera (£28m), Luke Shaw (£27m), Marcos Rojo (£16m), Daley Blind (£13.8m) na Pia kutumia £6m kumchukua Radamel Falcao kwa Mkopo.
No comments:
Post a Comment