BUKOBA SPORTS

Thursday, November 6, 2014

KOCHA MANUEL PELLEGRINI YUPO HALI TETE! NI BAADA YA CITY KUTUPWA MKIANI "KUNDI E"

BAADA ya Jana Mabingwa wa England Manchester City kutandikwa Bao 2-1 wakiwa kwao Etihad na CSKA Moscow na kutupwa mkiani mwa Kundi E la UEFA CHAMPIONS hali sasa Klabuni humo ni ya wasi wasi mtupu na hasa hatima ya Meneja wao Manuel Pellegrini.
Kwenye Kundi E, Man City wamebakiza Mechi 2 dhidi ya Bayern Munich Uwanjani Etihad na AS Roma huko Rome na hata wakishinda Mechi hizo inawezekana pia wasifuzu.
Lakini pia kwenye Mechi na Bayern Munich, Man City watawakosa Wachezaji wao wawili Fernandinho na Yaya Toure ambao walitwangwa Kadi Nyekundu kwenye Mechi na CSKA Moscow.

Akielezea yaliyowakuta, Manuel Pellegrini amesema Wachezaji wake wameshindwa kujiamini: “Ni kukosa kujiamini na inabidi tutafute sababu kwa kuongea nao kila Siku. Lazima tujue kwa nini Timu hii haifanyi vizuri kwenye UCL. Hawa ni Wachezaji muhimu sasa sielewi kwa nini wasicheze vizuri Ulaya. ”
Hata hivyo, Pellegrini amesisitiza hawawezi kukata tamaa ya kutofuzu wakati kimahesabu uwezo upo.
Nae Kepteni wa Manchester City Vincent Kompany alimuunga mkono Meneja wake ambae pia alikataa kutaja sababu ya kufungwa kwao ni Refa kutoka Ugiriki, Tasos Sidiropolous, ambae kwenye Mechi hiyo alifanya kosa la kutompa Kadi ya Njano Pontus Wernbloom kwa kosa alilofanya na badala yake kutoa Kadi ya Njano kwa Mchezaji mwingine kimakosa na kumnusuru Wenbloom kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Vile vile Mchezaji wa City Sergio Aguero, Uwanjani alilalamikia kunyimwa Penati mbili.
Pellegrini alieleza: “Kufungwa kwetu si Refa tu. Sitaki kutoa visingizio. Muhimu kwangu ni kuchunguza kwa nini hatuchezi kama kawaida tunavyocheza.”

Kuhusu Kadi Nyekundu aliyopewa Yaya Toure kwa kumsukuma usoni Roman Eremenko, Mchezaji huyo kutoka Ivory Coast ameelekea kuikubali baada ya kuibukia kwenye Mtandao wa Twitter akiwaomba radhi Mashabiki wa City.Timu Kepteni wa Man City  Vicent Kompany akilalamika kwa Waamuzi Mwamuzi Tasos akileza jamboSamir Nasri, Zabaleta, Aguero nao walitimba Waamuzi baada ya mtanange kumalizika kwa kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa CSKA Moscow

No comments:

Post a Comment