BUKOBA SPORTS

Sunday, November 23, 2014

LA LIGA: LIONEL MESSI AVUNJA REKODI YA UFUNGAJI BORA, BAADA YA KUPIGA HAT-TRICK!


Lionel Messi alipiga Bao 3 wakati Timu yake Barcelona ikiitwanga Sevilla Uwanjani Nou Camp Bao 5-1 kwenye Mechi ya La Liga na kuivunja Rekodi ya Mabao mengi ya Ligi hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na Fowadi wa Athletic Bilbao Telmo Zarra.
Zarra alikuwa ndie Mfungaji Bora huko Spain na Bao 3 za Messi zimemfanya afikishe Mabao 253 katika Mechi 289 za La Liga.
Telmo Zarra alifunga Mabao 251 katika Mechi 278 alizocheza kati ya Mwaka 1940 hadi 1955.
Katika Listi hiyo ya Wafungaji Bora wa Spain Mchezaji mwingine pekee ambae yumo katika 10 Bora na bado anaendelea kulisakata Soka lake huko Spain ni Mchezaji Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo, ambae ana Mabao 197 kwa Mechi 176.
Messi Akishangilia bao lake kabla ya mapumziko

Nimevunja Rekodi sasa!!

Mtanange ulivyokuwa ukiendelea kabla ya kufungana

Messi katikati akipongezwa na Vijana wenzake!

Taswira ya Mashabiki Uwanjani!

Sevilla hapa walipongezana baada ya kusawazisha!

Neymar nae alitupia

Neymar akishangilia

Kwa raha zao!

No comments:

Post a Comment