BUKOBA SPORTS

Saturday, November 8, 2014

LIVERPOOL 1 vs 2 CHELSEA, DIEGO COSTA AZIDI KUIPAISHA BLUES KILELENI!

Diego Costa akishangilia bao lake la kipindi cha pili dakika 67 na akiipandisha zaidi Chelsea kileleni wakiwa na pointi saba(7) kileleni.Gary Cahill(kushoto) akijipongeza huku kulia wachezaji wa Chelsea wakipongezana pia!!
Kipindi cha pili dakika ya 67 Diego Costa ndie aliyewapachikia bao Chelsea na kufanya 2-1 dhidi ya Wenyeji Liverpool kwenye Uwanja wao Anfield.Patashika kwenye Lango la Liverpool.
Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa sare ya bao 1-1Kipindi cha kwanza Liverpool wakiwa nyumbani Anfield ndio walianza kupata bao kupitia kwa Emre Can baada ya kupata ushirikiano kutoka kwa Raheem Sterling na kufanya 1-0 katika dakika ya 9 kipindi cha kwanza. Bao la Chelsea lilifungwa na Gary Cahill na kusawazsha bao hilo kwa kufanya 1-1. VIKOSI VINAVYOANZA:
CHELSEA 
Courtois; Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta; Matic, Fabregas; Ramires, Oscar, Hazard; Diego Costa.
LIVERPOOL 
Mignolet; Johnson, Skrtel, Lovren, Moreno; Gerrard, Can, Henderson; Coutinho, Balotelli, Sterling

No comments:

Post a Comment