
Danny Welbeck(kushoto) akishangilia bao lake la Ushindi baada ya kuifunga bao la pekee timu ya West Brom, Mtanannge uliomalizika kwa bao 1-0 jioni hii.

Danny Welbeck akiwafunga kwa kichwa West Brom baada ya kupokea krosi kutoka kwa Santi Cazorla katika dakika ya 60 kipindi cha pili.
Dakika ya 60 kipindi cha pili Danny Welbeck amewapa Ushindi Gunners kwa bao lake la kichwa baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa Santi Cazorla kama kona na hatimae kuruka juu na kuumalizia kwa kichwa hadi langoni mwa timu ya West Brom. Kipindi cha kwanza kilimalizika 0-0 licha kuwa na mshike mshike katika kipindi hichoi timu zote ziliweza kusakata kabumbu kwa makini.
VIKOSI:
Arsenal (4-2-3-1): Martinez; Chambers, Mertesacker, Koscielny, Monreal; Flamini, Ramsey; Welbeck, Alexis, Cazorla; Giroud.
AKIBA: Macey, Gibbs, Bellerin, Rosicky, Oxlade-Chamberlain, Campbell, Podolski.
West Brom (4-2-3-1): Foster; Wisdom, Lescott, Dawson, Pocognoli; Gardner, Mulumbu; Brunt, Dorrans, Sessegnon; Berahino.
AKIBA: Myhill, McAuley, Gamboa, Baird, Anichebe, Ideye, Samaras.
No comments:
Post a Comment