BUKOBA SPORTS

Saturday, November 29, 2014

COSAD YAANDAA SIKU YA KUAGA MWAKA NA KUPONGEZA WAFANYAKAZI (EMPLOYEES APPRECIATIONS DAYS).

Na Faustine Ruta, Bukoba
Mkurugenzi wa COSAD Tanzania, Bw. Smart Baitani akitoa neno mbele ya Wafanyakazi wake na Wageni wakati wa Tafrija fupi Kwa Mara ya Kwanza Katika Historia ya COSAD Tanzania iliandaa Chakula cha Jioni cha Kufunga mwaka na kupongeza Watumishi wake baada ya kufungua miradi Mikubwa Mitatu muhimu ( Clinic, Recording Studio na Biz Center) iliyofana na kuhudhuria na Washahuri mbali mbali toka sehemu mbali mbali ndani ya Mkoa na nje ya Mkoa wa Kagera.
Mkurugenzi wa COSAD Tanzania, Bw. Smart Baitani kutoka shirika lisilo la Kiserikali COSAD ambalo limezindua Miradi yake katika Manispaa ya Bukoba akiendelea kutoa neno mbele ya Wageni waliohudhuria siku hiyo ya kuaga Mwaka na kuwapongeza Wafanyakazi wa Cosad. Shirika la COSAD ambalo linatoa huduma za Kijamii, kama Hospitali, kituo cha Kibiashara, Klinik ya vitabu na ufugaji wa mbuzi, ambapo sasa uzinduzi wa Kliniki ya kisasa kabisa na studio ya muziki vilizinduliwa na Balozi wa Marekani Nchini.Miss Micky Donan(kulia) toka Ubalozi Mareakani ambaye anajitolea kama Profesor Katika Chuo Kikuu cha SAUT Bukoba nae pia alihudhuria hafra hiyo.Wakifurahia neno kutoka kwa Bw. Smart BaitaniMkurugenzi wa COSAD Tanzania, Bw. Smart Baitani alitambulisha Wafanyakazi wake.
Karibu sana!
Hii ndio "Kufana kwa siku ya wafanyakzi COSAD Tanzania" COSAD Annual Employees Appreciation Day/Night. Wakipata huduma ya Chakula cha usiku.Micky Donan akibadilishana mawazo na Mr. Bube Mkurugenzi wa Shule ya Leo leo wakati wa Msosi wa Pamoja wa Usiku.Baadhi ya wafanyakazi wa Cosad(kulia) ni dada Monica Paulo.
Wakiendelea kupata chakula cha Usiku
Mr. Bube
Bw. Baitani akiwa kwenye picha ya pamoja na Familia
SOMA ZAIDI HAPA CHINI

 Dada wa Cosad akitokelezea..
Miss Micky Donan(kulia) toka Ubalozi Mareakani ambaye anajitolea kama Profesor Katika Chuo Kikuu cha SAUT Bukoba akiwa anateta jambo na Mratibu wa Miradi Nchini Brittany Leitch.
Wakibadilishana Mawazo.
Mratibu wa Miradi Nchini Brittany Leitch akiwa(kushoto) akiwa na Monica Paulo
Bw. Ansbert Ngurumo(kutoka Mwandishi kutoka Gazeti la Tanzania Daima) rafiki yake na Bw. Smart Baitani  nae alikuwepo katika usiku huo na hapa alikuwa akitoa neno kuhusu Shirika hilo la CASAD.
Mwalimu Bube kutoka Shule ya Leo leo ya Hapa Bukoba(kulia ) akiteta na Mke wa Bw. Baitani
Dr. Erasmus Emmanuel(kushoto)
Marafiki: Bw. Smart Baitani na rafiki yake Ansbert Ngurumo(katikati).
Uende salama Mama!

Micky Donan nae alimuaga Bw. BaitaniKwenye UkodakMr. Bube akimuaga Mkurugenzi wa Cosad Bw. Smart Baitani Uende salama mkuu!!! Bw. Bube akimtakia safari njema Bwana Baitani ya kuelekea USA.

Picha ya pamoja ilipigwa!Karibu Cosad. Tuna miradi Mikubwa Mitatu muhimu ( Clinic, Recording Studio na Biz Center) Cosad ni shirika lisilo la serikali Tanzania wanaweka histori mpya yakufungua miradi katika upande wa afya kwa kufungua Zahanati katika katika Mkoa wa Kagera.

No comments:

Post a Comment