BUKOBA SPORTS

Monday, November 3, 2014

MASHINDANO YA PIKIPKI MKOANI KAGERA YAFANA!

Wakaazi wa Mji wa Bukoba na Wilaya Zake walijitokeza kwa wingi Jumapili tarehe 2.11.2014 kushuhudia Mashindano yaliyozikutanisha timu za Wilaya mbalimbali hapa Mkoani Kagera. Mashindano hayo yaliyokuwa yameratibiwa na Chama cha Sanaa Kagera The Amplified" yalichukua sura mpya baada ya Waendasha pikipiki hao kutoka katika Wilaya mbalimbali kama Ngara, Muleba, Biharamulo, Misenyi na Bukoba mjini na kuonesha kiwango kizuri kwani walikuwa ndio mashindano yao ya Kwanza. Mashindano hayo yalisindikizwa na Vijana Waendesha Pikipiki Kutoka Nchi Jilani Uganda. Katika Mashindano hayo Waganda ndio walianza kuendesha pikipiki hizo na kisha kuwaachia Watanzania waliokuwa tayari wameratibiwa kwa Mashindano hayo. Mshindi wa Kwanza alijinyakulia zawadi ya pesa laki 5, wapili laki 3 na watatu alipewa laki 2.
Mashindano  yakiendelea...





Hewani hewani baada ya kuruka tuta wakati wa mazoezi ya waendesha Pikipiki yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba.

Akiruka Gari
Akiwa hewani baada ya kuruka Gari

Wadau mbalimbali walijitokeza kushuhudia Mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba Jumapili 2.11.2014 kuanzia mchana.
Meza Kuu(kushoto) ni Willy O. Ruta akitazama Mashindano hayo kwa makini




Waandaaji wa Mashindano hayo ya pikipiki Bw. PK na (kulia) ni Bwana Tumaini.


No comments:

Post a Comment