BUKOBA SPORTS

Tuesday, November 11, 2014

MKUTANO WA TCRA NA (BLOGGERS) TANZANIA WAFANA MLIMANI CITY JIJINI DAR LEO.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene akitoa hotuba yake wakati akifunga Mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini na wamiliki wa Blogs (Bloggers) Tanzania uliokuwa na lengo la kutoa mafunzo ya namna ya kutoa taarifa mbali mbali wakati wa Chaguzi mbali mbali hapa nchini,unaoendelea kufanyika hivi sasa katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam.

Moja ya Mada zinazoendeleo kutolewa katika Mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Prof. John Nkoma akitoa hotuba yake wakati wa ufungumzi wa Mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini na wamiliki wa Blogs (Bloggers) Tanzania wenye lengo la kutoa mafunzo ya namna ya kutoa taarifa mbali mbali wakati wa Chaguzi mbali mbali hapa nchini,uliofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam.Picha na Othman Michuzi.

Inginia Andrew Kisaka akitoa Mada katika Mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini na wamiliki wa Blogs (Bloggers) Tanzania wenye lengo la kutoa mafunzo ya namna ya kutoa taarifa mbali mbali katika wakati wa Chaguzi mbali mbali hapa nchini.
Afisa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mabel Masasi akizungumza katika Mkutano huo.Taswira wamiliki wa Blogs (Bloggers) Tanzania wakisikiliza neno kutoka kwa Afisa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mabel Masasi 
Blogger Faustine Ruta(kushoto) kutoka www.bukobasports.com nae alikuwepo Ukumbini hapo  Mlimani City. Takribani Wanablog karibu 200 walihudhuria Mkutano huo Mlimani City leo hii.Mmiliki wa Blog ya 8020 fashion, Bi Shamim Mwasha akiuliza swali wakati wa mkutano wa bloggers uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani city leo.Wana Blog wakikazana kuchukua picha.Muda wa msosi uliwadia Maongezi ya hapa na pale yakapita!!! Faustine Ruta(kulia) akiteta na Mdau Othumani Michuzi. Pembeni ni mmiliki wa Kajunason Blog.

No comments:

Post a Comment