BUKOBA SPORTS

Tuesday, November 25, 2014

MMILIKI WA ARSENAL ALISHER USMANOV AMJIA JUU MZEE WENGER! AMTAKA ABADILIKE NA KUSAHIHISHA MAKOSA MARA MOJA!

Mmiliki wa Arsenal ambae ni wa Pili kwa wingi wa Hisa zake, Alisher Usmanov, amedai msimamo wa Meneja wao Arsene Wenger ndio unazuia Klabu hiyo kupanda juu na sasa inabidi Meneja huyo akiri makosa yake.
Usmanov, Raia wa Uzbekistani anaemiliki Asilimia 30 ya Hisa za Arsenal ambazo ni za pili kwa wingi wake, ameongea mara baada ya Klabu yao kuchapwa 2-1 na Manchester United hapo Jumamosi Uwanjani kwao Emirates.

Arsenal sasa wamepoteza Mechi 11 kati ya 15 walizocheza mwishoni na Man United na kushinda moja tu na Msimu huu kwenye Ligi Kuu England wameshinda Mechi 4 tu kati ya 12 walizocheza.

Usmanov ametamka: “Uwezo wa Timu upo lakini hamna mchanganuo wa kitaalam wa makosa yetu na kuyakubali. Hakuna mwerevu yeyeto anaeweza kudumu ikiwa hakubali makosa yake. Pale ukikubali makosa yako ndio unayaondoa. Nataka hili kwa Klabu yangu!”

Aliongeza: “Tunarudia yale yale Mwaka hadi Mwaka. Tuko juu kufuzu kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI lakini kila mara tunatolewa Raundi ya Mtoano tu. Nikiwa mwekezaji sifurahii hilo. Napenda msimamo wa Wenger. Lakini misimamo ni kizuizi. Na vizuizi Siku zote ni njia potofu. Ndio maana Makocha wasiokuwa na misimamo wanakuwa Makocha wa Timu Bora!”

Usmanov alimalizia: “Maoni yangu, tena nayaweka bayana, tunahitaji kuimarisha kila pozisheni ili tuwe sawa na Chelsea na Man City hapa England na Ulaya sawa na Real, Barcelona, Paris Saint-Germain, Bayern Munich na Klabu nyingine!”

No comments:

Post a Comment