BUKOBA SPORTS

Tuesday, November 18, 2014

RATIBA: MECHI KIMATAIFA ZA KIRAFIKI - LEO JUMANNE USIKU NI PATASHIKA SCOTLAND vs ENGLAND, PORTUGAL KUUMANA NA ARGENTINA OLD TRAFFORD!

NAHODHA wa England Wayne Rooney amewapoza Wachezaji Vijana wa England na kuwataka wasipate mchecheto kucheza ndani ya Celtic Park Jijini Glasgow Jumane Usiku mbele ya Mashabiki wa Wapinzani wao wa Jadi Scotland.
Rooney, ambae Jumamosi aliisawazishia England kwenye Mechi ya Kundi lao la EURO 2016 walipotoka nyuma na kuitwanga Slovenia Bao 3-1, ameshawahi kucheza Celtic Park mara mbili akiwa na Manchester United na anao uzoefu wa Mashabiki wenye kutia hofu wa Scotland.
Kutokana na upinzani mkubwa na wa Kihistoria kati ya England na Scotland ambao umesababisha hata Polisi wa pande zote mbili, England na Scotland, kuweka tahadhari kubwa kwenye Mechi hiyo, Rooney amewataka Wachezaji wa England kutulia.
Ametoa nasaha zake: “Hujui jinsi upinzani ulivyo hadi unapoingia Uwanjani na kupata uhalisi wa kelele na kila aina ya ushabiki. Inabidi Wachezaji wajue kupuuza upinzani huo wa Mashabiki na kutulia kucheza Soka lao la kawaida. Wasijihusishe.”
Kwenye Mechi yao ya mwisho England na Scotland kukutana, England iliichapa Scotland Bao 3-2 Uwanjani Wembley Jijini London Mwezi Agosti Mwaka Jana.
England watatinga kwenye Mechi hii bila Kipa wao Nambari Wani baada ya Meneja Roy Hodgson kumruhusu Joe Hart kurudi Klabuni kwake Manchester City na kutoa nafasi kwa Kipa wa zamani wa Celtic, Fraser Forster, au Kipa wa West Bromwich Albion, Ben Foster, kucheza.
Scotland, chini ya Kocha Gordon Strachan, wanaingia kwenye mtanange huu wakitoka kuwafunga Republic of Ireland Bao 1-0 kwenye Mechi ya Kundi lao la EURO 2016.
MECHI KIMATAIFA ZA KIRAFIKI
Jumanne Novemba 18

RATIBA/MATOKEO
Japan 2 v 1 Australia

19:00 Slovakia v Finland
20:00 Belarus v Mexico
20:00 Greece v Serbia
20:00 Slovenia v Colombia
21:00 Austria v Brazil
21:30 Romania v Denmark
22:30 Hungary v Russia
22:45 Italy v Albania
22:45 Poland v Switzerland
22:45 Portugal v Argentina
22:45 Rep of Ireland v USA
22:45 Spain v Germany
23:00 France v Sweden
23:00 Scotland v England

No comments:

Post a Comment