BUKOBA SPORTS

Tuesday, November 18, 2014

LEO NI PATASHIKA UWANJANI ESTADIO DE BALAIDOS KATI YA SPAIN vs GERMAN, NANI KUMKOMESHA MWENZAKE?

USIKU huu huko Mjini Vigo, Spain, Uwanjani Estadio de Balaídos, ipo Mechi ya Kimataifa ya Kirafiki kati ya Mabingwa wa zamani wa Dunia Spain na Mabingwa wa sasa wa Dunia Germany. Licha ya Germany kutwaa Ubingwa Mwezi Julai huko Brazil kwa kuifunga Argentina Bao 1-0, Mabingwa hao wa Dunia chini ya Kocha wao Joachim Low, wamekuwa hafifu baada ya ya kushinda Mechi mbili tu kati ya 5 walizocheza na kufungwa Mechi 2 dhidi ya Argentina, kwenye Mechi ya Kirafiki, na Poland, kwenye Mechi yao ya Kundi lao la EURO 2016.
Hali hii imemfanya Kocha Low kupiga mbiu kuwataka Wachezaji wake wa Germany wamalize Mwaka 2014 kwa kishindo kwa kuifunga Spain. 
Hata hivyo kazi hiyo inaelekea kuwa ngumu kwani Germany itawakosa Kipa wao Manuel Neuer, Andre Schurrle, Marco Reus, Christoph Kramer na Jerome Boateng kwani wote ni majeruhi. Lakini licha ya Spain, chini ya Kocha Vicente del Bosque, kuwakosa Mastaa wao Straika Diego Costa na Cesc Fabregas kutokana na kukabiliwa na maumivu, historia ya hivi karibuni pia uko upande wao kwani Spain imeifunga Germany mara 3 mfululizo kwenye Mechi zao za mwisho. Hata hivyo, katika Jumla ya Mechi zao 21 walizokutana, Germany wameshinda mara 8 na Spain kushinda mara 7.

No comments:

Post a Comment