BUKOBA SPORTS

Tuesday, December 9, 2014

BUNGE LA TANZANIA NA KENYA NGOMA YAMALIZIKA KWA SARE


Wachezaji wa Tanzania na Kenya wakiwa katika mashindano ya wabunge wa jumuiya ya Afrika mashariki leo, katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume jijini Arusha, mechi hiyo ilivuta hisia za wakazi wa jiji hilo waliomiminika kuja kushuhudia wabunge hao wakimenyana uwanjani, baada ya dakika ya tano bunge la kenya walijipatia bao la kwanza, bao lililofungwa na Mh.Steven Nyatta na hatimaye Tanzania kusawazisha dakika ya 24 kwa njia ya penalt baada ya Mh.Mbunge Joshua Nassari kudondoshwa eneo la hatari kwa kugongwa na mlinda mlango wa kenya Kega Kanin

Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mh Iddi Azan mlinda malango ambaye pia ni kiongozi wa timu ya bunge la Tanzania akinyaka magoli akionyesha umahiri wake wa kudaka mpira hali iliyosababisha mashabiki wa jiji la Arusha kumshangilia

Mlinda mlango wa Timu ya kenya Kega Kanin akijaribu kuzuia goli lililopatikana kwa njia ya penalt katika dakika ya 24

Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima akichechemea uwanjani baada ya kuanguka na kupewa huduma ya kwanza

Muonekano jukwaa kuu

Wachezaji wa timu ya Tanzania wakijadiliana uwanjani kabla ya mechi kuanza

Wachezaji wa timu ya Kenya wakijadiliana uwanjani kabla ya mechi kuanza

Kushoto ni mchezaji wa timu ya kenya Mh.Peter Kaluma katikati ni Mh Dan Wanyama wa kenya mrefu kuliko wote uwanjani alipewa kadi nyekundu baada ya kuonekana akijibizana na mwamuzi aliyekuwa akichezesha mpambano huo kulia ni Mh Joshua Nassari wa Tanzania


Kushoto Mh Iddi Azan ambaye ni mlinda malango wa timu ya Tanzania akiwa katika mapumziko, aliyeshikilia mpira ni mwamuzi wa mpambano huo Erick Onoko

Mh Joshua Nassari wa Tanzania akipewa huduma ya kwanza

Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima akipatiwa huduma ya kwanza

Mh.Mbunge wa Tanzania akiwa amelala chali akionekana kuwa na maumivu makali baada ya kuumia katika mechi hiyo wabunge wenzake wakijaribu kumsaidia

Mashabiki wa Kenya wakiwa wanashangilia huku wakiwa wanaonyesha bwebweeee zao

Umati wa watu waliokuja kushuhudia mpambano wa Tanzania na Kenya

Mashabiki wa Tanzania wakiwa wanashangilia kwa kuzunguka uwanja

Watoa huduma ya kwanza kutoka msalaba mwekundu wakiwa wanafatilia mechi ya wabunge wa Afrika mashariki.(Habari Picha na Pamela Mollel wa Jamiiblog Arusha)

No comments:

Post a Comment