BUKOBA SPORTS

Monday, December 15, 2014

KOCHA WA UNITED LOUIS VAN GAAL AKWEPA SWALI LA KUSAKA UBINGWA!! AANGALIA MBELE DHIDI YA ASTON VILLA!

Louis van Gaal amegoma kujitumbukiza kwemye mjadala kuwa Timu yake Manchester United sasa wamo rasmi kwenye mbio za Ubingwa baada ya Jana kuwabamiza Mahasimu wao wa Jadi Liverpool Bao 3-0 Uwanjani Old Trafford kwenye Mechi ya Ligi Kuu England. Bao za Jana zilifungwa na Wayne Rooney, Juan Mata na Robin van Persie.
Man United wapo Nafasi ya 3 kwenye Ligi wakiwa Pointi 5 nyuma ya Timu ya Pili Man City na Pointi 8 nyuma ya Vinara Chelsea. Lakini Van Gaal alikataa kutamka wazi kama wapo kwenye kinyang’anyiro cha mbio za Ubingwa na badala yake kusema: “Nimefurahi sana lakini Mechi ijayo, dhidi ya Aston Villa, ndio muhimu. Ni Mechi ya Ugenini na tuna matatizo na Mechi za Ugenini.” Licha ya kushinda Mechi 6 mfululizo kwenye Ligi, Van Gaal anaamini Timu yake inabidi ifanye vyema zaidi na alihuzunishwa na kuipa Liverpool nafasi nyingi za kufunga na kumfanya Kipa David De Gea aibuke shujaa kwa kuokoa Goli za wazi karibu 4 au 5. Van Gaal ameeleza: “Nimeridhika na matokeo. Tulipoteza Mipira mingi kipuuzi na kuwapa Liverpool nafasi nyingi za kushambulia. Nitahoji Wachezaji kwanini!”

No comments:

Post a Comment