BUKOBA SPORTS

Saturday, December 6, 2014

USAJILI: NYOSSO AJIUNGA NA MBEYA CITY!

BEKI wa zamani wa Simba, Juma Nyosso, amejiunga na Mbeya City FC na kusaini Mkataba wa Mwaka mmoja.
Kwa mujibu wa Tovuti ya Klabu ya Mbeya City, Nyosso, ambae pia aliwahi kuzichezea Ashanti na Coastal Union, amesema amesaini Mkataba wa Mwaka mmoja akiamini kuwa utamtosha kuishawishi Mbeya City kumpa Mkataba mrefu zaidi.

Nyosso alisaini Mkataba wake kwenye Ofisi za Mbeya City zilizopo Jengo la Mkapa Hall Jijini Mbeya na amesema: “City ni Timu nzuri na imekuwa hivyo toka ilipoanzishwa Miaka minne iliyopita. Matokeo yaliyopo sasa ni sehemu ya Soka ambayo Timu yoyote inaweza kuyapata, nimekubali kujiunga na Timu kwa Mkataba wa Mwaka mmoja kwa sababu naamini uwezo wangu Uwanjani utawashawishi Viongozi kunipa mkataba mrefu zaidi pindi huu utakapomalizika na ninaamini hili linawezekana kwa sababu nataka kukaa kwenye Timu hii mpaka mpira wangu utakapoisha.”
Nae Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, akiungwa mkono na Kocha Mkuu Juma Mwambusi, amesema: “Tunamshukuru kukubali kujiunga nasi, imani yetu kubwa kwamba uzoefu alionao utasaidia kuimarisha safu yetu ya ulinzi, hasa ukizingatia matokeo tuliyopata katika michezo saba ya mwanzo wa Ligi hii”
Tayari Nyosso amejiunga na Kikosi cha Mbeya City kilichosafiri kwenda mjini Songea kwa Mechi za Kirafiki.

LIGI KUU VODACOM
RATIBA
Ijumaa Desemba 26

Simba v Kagera Sugar


Jumamosi Desemba 27
Mtibwa Sugar v Stand United
Prisons v Coastal Union
JKT Ruvu v Ruvu Shootings

Jumapili Desemba 28
Mbeya City v Ndanda FC
Polisi Moro v Mgambo JKT
Yanga v Azam FC

No comments:

Post a Comment