BUKOBA SPORTS

Saturday, December 6, 2014

VAN GAAL AWATULIZA WAANDISHI WA MAGAZETI KUHUSU KUNUNUA WACHEZAJI!


Meneja wa Man United Van Gaal ameshambulia Magazeti ya Uingereza kwa kuandika kuwa amepewa kitita cha Pauni Milioni 100 kununua Wachezaji wapya ili kuimarisha Kikosi chake.
Van Gaal amewaambia Waandishi kuwa stori za aina hiyo zitaathiri wao wakitaka kununua Wachezaji.

Akiongea na Wanahabari kwenye Mahojiano maalum kwa jili ya Mechi ijayo ya Ligi na Southampton, Van Gaal alitamka: “Nadhani inachefua kuandika namba. Sidhani Ed Woodward [Makamu Mwenyekiti Mtendaji] amesema kuhusu hilo na mimi sijasema.”
Aliongeza: “Ni kuvunja heshima kwa Wachezaji wangu na sitaki kuongea hilo. Nawaamini Wachezaji wangu na tutafanya kazi pamoja!”

Van Gaal pia aliwapasha Waandishi hao kwa kuwaambia Man United haina tatizo la pesa bali wakiingia Sokoni ndio dau huzidi.
Alinena: “Unadhani Southampton inalipa Fedha nyingi kwa Wachezaji wake? Sidhani kwa sababu ni Southampton. Kuna uhusiano Real Madrid na Man United na si Aston Villa na Southampton. ” Wanahabari hao pia walikumbusha bifu lake na Ronald Koeman Meneja wa sasa wa Southampton ambayo watakutana nayo Mechi ijayo ya Ligi Jumatatu Usiku.

No comments:

Post a Comment