Cordoba walipata bao mapema kuptia kwa Nabil Ghilas aliyeipachikia bao la mapema dakika ya 3 kwa mkwaju wa penati.
BAO za Real Madrid zilifungwa dakika 27 na Karim Benzema kipindi cha kwanza na lile la dakika za majeruhi la Gareth Bale dakika ya 89 kwa mkwaju wa penati. Mpira huo haukumalizika vyema Real Madrid walipata balaa pale Staa wao Cristiano Ronaldo alipooneshwa kadi Nyekundu.
Real Madrid wamepata ushindi huu kwa jasho wa Bao 2-1 walipocheza Ugenini huko Estadio Nuevo Arcángel Mjini Córdoba kwa kuichapa Cordoba huku Bao la ushindi likifungwa Dakika ya 89 kwa Penati ya Gareth Bale.
Real walicheza Mtu 10 kuanzia Dakika ya 82 kufuatia Kadi Nyekundu kwa Mchezaji Bora Duniani, Cristiano Ronaldo, kwa kuinua mkono wake na kudaiwa kumpiga usoni Edimar.
Cordoba ndio waliotangulia kupata Bao katika Dakika ya Pili tu kwa Penati ya Ghilas baada ya Sergio Ramos kuunawa Mpira lakini Karim Benzema akaisawazishia Real katika Dakika ya 27.
Ushindi huu umewapaisha Real kuwa Pointi 4 mbele ya Timu ya Pili Barcelona huku wote wakiwa wamecheza Mechi sawa ingawa Barcelona baadae leo watacheza Mechi yao ya La Liga Ugenini na Elche.
No comments:
Post a Comment