
Full Time: 4-2 Chelsea watupwa nje FA CUP.
Chelsea waliongoza Bao 2-0 lakini Bradford City, inayocheza Ligi 1 ikiwa ni Madara mawili chini ya Chelsea, ilizinduka na kupiga Bao 4.
Chelsea walitangulia kwa Bao za Garry Cahill na Ramires na Stead kuipa Bao 1 Bradford kabla ya Kipindi cha Kwanza kumalizika.
Kipindi cha Pili, Bradford walipiga Bao 3 kupitia Morais, Mchezaji wa zamani wa Chelsea, Halliday na Yeates. 
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho akionekana kuwa na wasiwasi baada ya kutolewa kwenye FA CUP na timu ndogo ya Bradford kwa kuchabangwa bo 4-2. Chelsea ndio inaongoza Ligi Kuu England kwa msimu huu 2014/15 ikiwa Kileleni.
Huko Etihad, Mabingwa wa England, Manchester City, walipigwa Bao 2-0 na Middlesbrough inayocheza pia Daraja la chini Championship kwa Bao za Kipindi cha Pili za Bamford na Garcia Martinez.
Baadhi ya Wachezaji wa Chelsea wakio hoi baada ya kuchapwa na kutupwa nje FA CUP

Bradford wakishangilia Ushindi
No comments:
Post a Comment