BUKOBA SPORTS

Thursday, January 22, 2015

FRIENDLY MATCH: TAIFA STARS MABORESHO 1 vs 1 RWANDA, HAKUNA MBABE AMAVUBI WAKOMALIWA NA VIJANA WA BONGO KWA SARE!


Nahodha wa Taifa Stars Simon Msuva (kushoto) akibadilishana bendera na nahodha wa timuya taifa la Rwanda 'Amavubi' Haruna Niyonzima (kulia) kabla ya mpambano wa kirafiki uwanja wa CCM Kirumba Mwanza. Hadi mwisho wa mchezo timu zinatoka sare ya kufungana bao 1-1.

Kikosi cha Taifa Stars 'Maboresho' kilichoshuka leo dimba la CCM Kirumba kukiputa na Amavubi.

Timu ya taifa la Rwanda aka 'Amavubi'

Rais wa TFF Malinzi (wa tano toka kushoto) akiwa na safu ya wakuu meza kuu wakati wimbo wa taifa la Rwanda ukipigwa.

Rwanda.

Mgeni rasmi Mkurugenzi wa MWAUWASA Anthony Sanga akipata utambulisho toka kwa nahodha wa Taifa Stars Simon Msuva (kulia) ambaye hapa akimtambulisha golikipa wa Stars Manyika Peter.

Mgeni rasmi Mkurugenzi wa MWAUWASA Anthony Sanga akipata utambulisho toka kwa nahodha wa Rwanda Haruna Niyonzima (kulia) ambaye hapa akimtambulisha golikipa wa Amavubi Oliver Kwizera.

Nahodha wa Stars Simon Msuva (kushoto) akiukokota mpira kulia mwa uwanja kuelekea goli la Rwanda mbele ya Mugeraneza Batist ambaye ndiyo mfungaji wa bao la Rwanda katika mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki ulio katika Kalenda ya FIFA ukifanyika dimba la CCM Kirumba Mwanza. Hadi mwisho Tanzania na Rwanda zinatoka sare ya 1-1.

Simon Msuva akihaha winga ya kushoto kuelekea lango la Amavubi Rwanda nyuma yake ni beki namba mbili Baysenga Emiry (15) na kwa umakini golikipa wa Rwanda Oliver Kwizera (18) akifuatilia mwenendo wa ulinzi.

Hili ndili goli la kuongoza la Rwanda likifungwa kwa kichwa dakika ya 9 ya mchezo na Mugeraneza Batist, golikipa kupitia mpira wa kona, naye golikipa wa Stars Manyika akiwa ametoka kuuokoa mpira huo alirudi golini kinyumenyume akiushuhudia ukitikisa nyavu zake .

Mpira unazama kimiani ....Rwanda inapata bao la kuongoza.......

Kutoka kushoto ni Sibomana Patrick (Rwanda), katikati ni Shiza Rama (Tanzania), Mugeraneza Batist, Bigirimana Issa na Ismail Nshatyamagara wote wa Rwanda.

Patashika langoni mwa Rwanda toka winga ya kushoto.


Faustine Ruta Hakuna mbabe kati ya Taifa Stars maboresho na Amavubi ya Rwanda hapa jijini Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba.Dakika zinayoyoma...zikiwa zimebaki nakika 9 tu...

Kelvin Friday anapumzishwa na nafasi yake inachukuliwa na Mchezaji Rashid Mandawa anayekipiga katika Klabu ya Kagera Sugar.

Kocha wa Timu ya Rwanda ni Briton Lee Johnson. Kelvin Friday anaisawazishia bao Taifa Stars Maboresho katika dakika za lala salama za kipindi cha kwanza akifunga bao hilo dakika ya 45 na kuongezwa muda wa nyongeza dakika 4. 

Taifa Stars Maboresho bao hilo la kusawazisha linawapa nguvu na kuchangamka..
Vikosi vya Stars na Amavubi vya leo vilikuwa:
Taifa Stars Maboresho: Manyika Peter, Miraj Adam, Gadriel Michael, Andrew Vicent, Joram Mgeveke, Salum Mbonde, Said Ndemla, Hassan Dilunga, Kelvin Friday, Simon Msuva na Shiza Ramadhan/ Salum Telela (dk 45).

Rwanda - Amavubi: Olvier Kwizera, Baysega Emiry, Ismail Nsutyamagara, Sekamana Mayime, Rusheshanganga Michael, Mugereneza Batist, Haruna Niyonzima, Bigirimana Issa, Sibomana Patric, Mutuma Janveer na Iradukunda Betrand.

No comments:

Post a Comment