Van Persie, mwenye Miaka 31, ameeleza: “Si juu yangu. Kwa sasa nabakia hapa hapa kwa Miezi 18. Huo ndio ukweli. Sijui baadae kuna nini. Sijui nini litatokea. Inabidi tungojee na kuona.”
Mbali ya kutokuwa na hakika kuhusu hatima yake, Van Persie, ambae ni Nahodha wa Timu ya Taifa ya Netherlands, amekiri kutokuwa na furaha na ufungaji wake Mabao Msimu huu ambapo amefunga Bao 8 katika Mechi 25 alizochezea Man United ambayo pia imekuwa ikisuasua katika ufungaji ikiwa imefunga Bao 5 tu katika Mechi zao 6 zilizopita.
Van Persie amesema Timu nzima lazima ibebe lawama licha ya kuwa Nafasi ya 4 kwenye Msimamo wa Ligi Kuu England.
Kwenye Msimu wake wa kwanza na Man United, ule wa 2012/13 ambao walitwaa Ubingwa, Van Persie alifunga Bao 30 na Msimu uliopita, ambao aliandamwa na maumivu ya mara kwa mara, alifunga Bao 18.
Mechi inayofuata kwa Man United ni ile ya Ligi Kuu England hapo Jumamosi Uwanjani Old Trafford dhidi ya Leicester City.
No comments:
Post a Comment