UHAMISHO: REAL MADRID YAMSAINI KIUNGO TOKA BRAZIL LUCAS SILVA.
Real Madrid wamekamilisha kumsaini Kiungo wa Timu ya Taifa ya Brazil ya Vijana U-21, Lucas Silva, kwa Dau la Euro Milioni 14 na kumpa Mkataba wa Miaka 5 na Nusu. Silva alikuwa akiichezea Klabu ya Cruzeiro huko kwao Brazil na anakuwa Mchezaji wa Pili kusainiwa na Real Mwezi huu Januari mwingine akiwa Kinda wa Miaka 16 kutoka Norway, Martin Odegaard, alienunuliwa kutoka Stromsgodset.Lucas Silva alikamilisha usajili huo jana Ijumaa.
No comments:
Post a Comment