BUKOBA SPORTS

Wednesday, February 11, 2015

AZAM FC WAREJEA KILELENI KWA KUIPA KIPIGO KIZITO MTIBWA SUGAR CHA BAO 5-2 CHAMAZI JIJINI DAR ES SALAAM.


Mabingwa watetezi Azam Fc wamerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Vodacom Premier Ligi baada ya kuifunga timu ya Mtibwa Sugar bao 5-2 leo kwenye Uwanja wa Chamazi Jijini Dar es salaam. Ushindi huu umeipandisha Azam Fc baada ya kucheza mchezo huo wa 13 wakiwa na kufikisha pointi 25 wakipishana kwa magoli ya kufunga na Timu ya Yanga kileleni.
Mabao ya Azam Fc leo yamefungwa na Kipre Tchetche, Frank Domayo na Didier Kavumbagu katika kipindi cha kwanza walichopumzika wakiongoza kwa goli 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar ya Mjini Morogoro.
Kipindi cha pili Azam Fc waliendelea na kasi na kuweza kufunga bao kupitia kwa Frank Domayo tena katik kipindi cha pili dakika ya 58 na Mtibwa walipambana na kupata bao la pili kupitia kwa Ame Ally akifahamika kwa jina la Zungu" katika dakika ya 70.
Kipre Tchetche alimaliza mchezo kwa kuichoma bao la tano Mtibwa Sugar katika dakika ya 86 na kufanya mtanange huo kumalizika kwa bao 5-2.
Mshambuliaji wa Azam FC, Salum Abubakar akimiliki mpira.
Frank Domayo (shoto) akichuana na beki wa Kagera Sugar, Mussa Nampaka.
Wachezaji wa Azam FC wakishangilia bao la kwanza la timu hiyo.
Kipre Tchetche akimiliki mpira.
Frank Domayo akishangilia bao lake.

Kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohamed akiokoa moja ya hatari langoni mwake.

No comments:

Post a Comment