BUNDESLIGA: VfB STUTTGART 2 vs 3 BORUSSIA DORTMUND
Bao za Borussia Dortmund zilifungwa na Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 25 Ilkay Gündogan aliwaongezea bao tena la pili dakika ya 39 na Dakika ya Lala salama Borussia Dortmund walipata bao la zawadi na la Ushindi dakika ya 89 baada ya kupata bao kupitia kwa Marco Reus dakika ya 89 baada ya mchezaji wa VfB Stuttgart kutoa pasi hewa na hatime Reus kupata mpira huo na kuziona nyavu kwa bao la tatu.
VfB Stuttgart walijitutumua na kupata bao la pili dakika ya 90 kupitia kwa Georg Niedermeier na lile la mkwaju wa Penati kipindi cha kwanza kusawazisha kuptia kwa Florian Klein dakika ya 32.
Ushindi huu wa Borussia Dortmund unawapandisha hadi nafasi ya 10 wakiwa na pointi 25 na wao VfB Stuttgar wanatupwa nafasi ya Mkiani wakiwa na pointi 18 tu katika michezo 22 walizocheza mpaka hii leo.
No comments:
Post a Comment