Chama cha kandanda mkoa wa Dar es salaam DRFA, kimeipongeza timu ya Temeke kwa kutwaa Ubingwa wa Taifa Wanawake,baada ya kuifunga Pwani kwa bao 1-0,kwenye mchezo wa fainali uliopigwa jumapili ya Januari 31 kwenye dimba la Azam Complez huko Chamazi.
Katika fainali hiyo iliyohudhuriwa na waziri mwenye dhamana ya michezo Dk.Fenella Mukangara,imeshuhudiwa Temeke ikijipatia bao lake mnamo dakika ya 66 kupitia kwa mchezaji wao Neema Paul.
Nahodha wa Timu ya Pwani akipokea Mfano wa hundi ya Shilingi Milioni Mbili ambazo ni zawadi ya Mshindi wa pili katika Mashindano ya Proin Women Taifa Cup na kuwamalizika kwa Temeke kuwa Mabingwa kwa kuifunga Pwani goli 1 kwa 0.
Nahodha wa Timu ya Ilala ambao ni washindi wa tatu akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni 1 ambayo mshindi wa tatu katika Mashindano hayo ni Ilala
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara (wa kwanza kulia) na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Jamal Malinzi wakishuhudia fainali ya Mashindano ya Proin Women Taifa Cup mechi iliyochezwa katika dimba la Azam Complex kwa kuzikutanisha timu za Pwani na Temeke na Temeke Kuibuka Bingwa wa Proin Women Taifa Cup kwa kuichapa Pwani goli 1 kwa 0.
Kikosi cha Timu ya Pwani
Kikosi cha Timu ya Temeke ambacho kimeifunga Kikosi cha Timu ya Pwani kwa goli 1 kwa 0 katika Mchezo wa Fainali ya Mashindano ya Proin Women Taifa Cup, mchezo uliomalizika kwa Temeke kuibuka mabingwa wa Proin Women Taifa Cup katika Dimba la Azam Complex
Waziri Mukangala akisalimiana na timu ya Temeke pamoja na timu ya Pwani kabla ya Mechi ya Fainali ya Proin Women Taifa Cup kuanza katika dimba la Chamanzi Complex. Temeke iliibuka Mshindi kwa kuifunga Pwani Goli 1 kwa 0Temeke walifanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kuwafunga ndugu zao Ilala kwa mabao 4-0,huku pwani wakitinga hatua hiyo kwa kuifunga Kigoma mabao 3-2,katika michezo ya nusu fainali.
Mshindi amejinyakulia kitita cha shilingi milioni tatu, makamu bingwa sh. milioni mbili, wakati mshindi wa tatu ameondoka na sh. milioni moja katika michuano hiyo.
Mbali na Temeke kubeba ubingwa huo,pia imefanikiwa kutoa mlinda mlango bora, Belina Julius aliyezawadiwa kitita cha shilingi 500,000/-.
Mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu uliwakutanisha, Ilala dhidi ya Kigoma ambapo ilala imefanikiwa kuchukua nafasi ya tatu baada ya kushinda mabao 3-0.Uongozi wa DRFA,unatoa shukurani kwa mashabiki wa mkoa wa Dar es salaam na maeneo ya jirani,ambao wamejitokeza kwa wingi kushuhudia michuano hiyo,na kuwaomba waendelee na mfumo huo ili kuleta hamasa kwa wachezaji.
No comments:
Post a Comment